SERIKALI
imesema kuwa haina mpango wakujenga nyumba za kuwapa Wananchi bure
kutokana na gharama ambazo Serikali inagharamia katika ujenzi nyumba
hizo.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Angeline Mabula (Pichani)wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la
Taifa(NHC).
Angeline
amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya
kuuzwa pamoja na kupangisha na si kuwapa wanchi bure.
Amesema
kuwa gharama ya kujenga nyumba hizo inakuja katika maandalizi ya ujenzi
ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu kama Barabara, Maji pamoja na
Umeme.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC),
Nehemia Mchechu amesema shirika hilo tayari limejenga nyumba za kutosha
katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.
Pia
amesema katika nyumba za mikoani shirika hilo limeuza nyumba hizo kwa
40% hadi 50% huku akisisitiza zaidi kuendelea na Kampeni ya (Nyumba
yangu, Maisha yangu) ili wananchi wawezi kumudu gharama za nyumba hizo.