Leo
ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman
Kova, kulitumika jeshi la Polisi nchini kwa kuwa muda wake wa
kulifanyia kazi jeshi hilo umeisha.
Kamanda Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumza katika
kipindi cha kumekucha cha ITV, na kusema kuwa mkataba wake na jeshi la
Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni.
"Mmepata
bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea
Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia
hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi,
mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi,
Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi", alisema Kamanda Kova.
Kamanda
Kova alikuwa Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, na kwa mujibu
wake amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya kiuhalifu,
yaliyokuwa yanaitikisa nchi hususani matukio ya wizi na uvamizi wa
kwenye benki.